Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sayyid Murtadha Kashmiri, mwakilishi wa Ayatollah Al-Udhma Sayyid Ali Sistani barani la Ulaya, katika ujumbe wake kwa mazuwari wa Arubaini amesisitiza kwamba: Ziara ya Arubaini si hafla ya kidini pekee, bali ni alama ya kimataifa ya uamsho, uaminifu wa haki na kupinga dhulma na uonevu.
Katika ujumbe huu, huku akibainisha maana halisi ya Ziara ya Arubaini na malengo yake ya juu kabisa, amerejelea fitna na mashambulizi ya kifikra na ya vyombo vya habari dhidi ya ziara hii kubwa, na amewalingania waumini wahifadhi na walinde harakati hii hai na takatifu.
Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sayyid Murtadha Kashmiri, katika sehemu ya ujumbe wake, huku akishukuru juhudi na ukarimu wa watu wa Iraq katika kuhudumia mazuwari, ameieleza Arubaini si tu kuifanya upya ahadi ya Mwenyezi Mungu isiyo na mipaka ya muda au ya kundi maalumu, bali ni sauti ya kimataifa kwa wote wanaotafuta uhuru duniani kote.
Mwakilishi wa Ayatollah Al-Udhma Sayyid Ali Sistani katika bara la Ulaya, akiendelea na ujumbe huu, ameongeza kuwa: "Imam Hussein (as) mpaka sasa bado anaendelea kudhulumiwa, na dhulma bado inaendelea", Enyi wapenda uhuru duniani! Simameni kuutetea ukweli, wala msitosheke na matembezi pekee; bali kwa nyoyo, akili, kalamu na mienendo yenu, kuweni walinzi wa ahadi hii tukufu, kila mtu anayepiga hatua kwa ikhlasi katika njia hii, ni kama tofali imara katika ukuta thabiti wa dini ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu daima atailinda dini yake, ijapokuwa makafiri hawapendezwi nayo.
Ameendelea kusisitiza kwamba Ziara ya Arubaini ya Husseini si ada ya kidini pekee, bali ni mimbari ya uamsho na mfano wa kivitendo wa Mapinduzi ya Husseini; taswira ya uaminifu kwa haki na kukanusha batili kwa namna ya pamoja na ya kijumla. Hii ndiyo sababu kwa karne nyingi ziara hii daima imekuwa shabaha ya mishale ya maadui na madhalimu, na kitovu cha mapambano ya kimaadili, kifikra na ya vyombo vya habari dhidi ya haki.
Aidha, amegusia matatizo na changamoto za kisasa zinazo ikabili ziara hii, ikiwemo upotoshaji, kuzusha sintofahamu, marufuku na propaganda zisizo sahihi ambazo mara kadhaa zimekuwa kizuizi katika njia hii ya Mwenyezi Mungu, na amewataka waumini walinde njia hii tukufu kwa umakini na kwa kutumia nyenzo sahihi.
Maoni yako